KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, October 8, 2012

YANGA YACHECHEMEA, YACHAPWA 1-0 NA KAGERA SUGAR





Bao lililofungwa na mashambuliaji Themi Felix leo limeiwezesha Kagera Sugar kuipiga Yanga mweleka wa bao 1-0 katika mechi ya ligi kuu ya Tanzania bara iliyochezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Felix alifunga bao hilo dakika ya 67 kwa shuti kali lililomshinda kipa Yaw Berko wa Yanga na kuwafanya mashabiki wa klabu hiyo kongwe nchini watoke uwanjani wakiwa wamenyong'onyea.
Kagera Sugar imekuwa timu ya pili kuipa kisago Yanga tangu ligi hiyo ilipoanza kutimua vumbi Julai mwaka huu. Yanga ilipata kipigo chake cha kwanza kwa kuchapwa mabao 3-0 na Mtibwa Sugar mjini Morogoro.
Yanga inatarajiwa kushuka tena dimbani Alhamisi kumenyana na Toto African mjini Mwanza.

No comments:

Post a Comment