KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, October 16, 2012

SIMBA, KAGERA SUGAR KAZI IPO KESHO



Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaingia raundi nane kesho (Oktoba 17 mwaka huu) kwa mechi tano huku vinara wa ligi hiyo Simba wakiialika  Kagera Sugar kutoka mkoani Kagera kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi hiyo namba 52 itachezeshwa na mwamuzi Ronald Swai kutoka Arusha wakati waamuzi wasaidizi ni Julius Kasitu na Methusela Musebula, wote kutoka Shinyanga. Mwamuzi wa akiba ni Ephrony Ndisa wa Dar es Salaam huku mtathimini wa waamuzi akiwa Charles Mchau kutoka Moshi.
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Tanzania Prisons inayofundishwa na Jumanne Chale na Azam iliyo chini ya kocha Boris Bunjak kutoka Serbia. Nayo Polisi Morogoro iliyopanda msimu huu itakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Jamhuri.
Mgambo Shooting ambayo imepata ushindi mara mbili mfululizo itakuwa nyumbani Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga ikiikaribisha Toto Africans katika mechi itakayochezeshwa na Geofrey Tumaini wa Dar es Salaam.
Oljoro JKT inayonolewa na Mbwana Makata itakuwa nyumbani Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha dhidi ya African Lyon.

No comments:

Post a Comment