MFADHILI wa zamani wa Simba, Azim Dewji amelitaka Shirikisho la SokaTanzania (TFF) na wadhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Kampuni yaSimu za Mkononi ya Vodacom kutotumia nguvu kubwa kulumbana na vilabukatika suala la udhamini. Akizungumza jana, alisema anashangazwa na mvutano unaoibuka kati yaTFF, wadhamini na baadhi za klabu zilizoingia mkataba na kampuni zingine za simu nchini, akisema klabu zina haki ya kujitafutia malishoya ziada. “Sioni tatizo ni nini kwa sababu wadhamini ni kwa ajili ya ligi, siklabu…ndiyo maana hata Uingereza, wadhamini wa Ligi Kuu ni benki yaBarclays, lakini klabu kama Liverpool zinadhaminiwa na benki yaStandard Chartered. “Angalia jezi za Liverpool, zina nembo kubwa kabisa kifuani, mbonahatusikii wakisumbuana?” anahoji Dewji aliyeifadhili kwa mafanikiomakubwa Simba, ikiwa pamoja na kuifikisha fainali za Kombe la CAFmwaka 1993. Aidha, mfanyabiashara huyo maarufu anaongeza kuwa, ifike mahali TFFiwe msaada kwa klabu zote nchini, akisema kwa kuzibana ni sawa nakudidimiza kiwango cha soka kwani kamwe hazitaweza kunufaika nalolote, zaidi ya nyingi kuishia kupanda daraja na kushuka kutokana naukata. “Ni klabu chache sana nchini zenye uhakika wa udhamini, labda Simba,Yanga na klabu za makampuni kama Azam, Mtibwa na Kagera Sugar. Je,hizi nyingine ambazo hazina mdhamini, baba wala mama zitajiendeshaje? “Nadhani kuna mahali panya mwanya, lazima warekebishe hali hii ilikila klabu iwe na maamuzi ya kutafuta mdhamini anayemtaka. Kudhaminiligi kiwe kitu kimoja na kudhamini klabu kitu kingine, ndivyo wenzetuwanavyofanya,” alisisitiza. Kauli ya Dewji imekuja siku chache tangu kuibuka kwa mvutano baina yawadhamini, TFF na klabu ya African Lyon ambayo katika kuhakikishainaendesha mambo yake, iliingia mkataba na kampuni ya simu za mkononiya Zantel, hali inayoelezwa kuleta mgongano wa kimaslahi.
'
Sunday, October 7, 2012
AZIM DEWJI ATOA SOMO KWA TFF, VODACOM

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment