KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, October 16, 2012

MBAGA KUZICHEZESHA KENYA NA AFRIKA KUSINI


Mwamuzi Oden Mbaga wa Tanzania anayetambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu  (FIFA) ndiye anayechezesha mechi ya kirafiki kati ya Kenya (Harambee Stars) na Afrika Kusini (Bafana
Bafana).
Mechi hiyo inachezwa leo Uwanja wa Kimataifa wa Moi Kasarani jijini Nairobi. Mbaga anasaidiwa na waamuzi wasaidizi wa FIFA, John Kanyenye kutoka Mbeya na Erasmo Jesse wa Morogoro.
TFF imeteua waamuzi hao baada ya kupata maombi kutoka kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kenya (FKF) ambao ndiyo waandaaji wa mechi hiyo ambayo ni moja ya vipimo kwa kocha mpya wa Harambee Stars, Henry Michel kutoka Ufaransa.

No comments:

Post a Comment