KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, May 29, 2012

Meneja aliyetimuliwa Twanga Pepeta atua Mashujaa

Aliyekuwa Meneja wa bendi ya Twanga Pepeta International, Martine Sospeter (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi kuhusu uamuzi wake wa kujiunga na bendi ya Mashujaa. Kushoto ni kiongozi na mwimbaji wa bendi hiyo, Charlz Baba na kulia ni mratibu na mwanzilishi, Dodoo La Bouche.


"Juzi usiku nilishangazwa na kauli ya mkurugenzi wangu wa zamani katika
Bendi ya African Stars,Asha Baraka katika vyombo mbalimbali vya habari
kuwa amenifukuza kazi kutokana kuhujumu bendi ikiwemo kushawishi
wanamuziki kujiunga na bendi ya Mashujaa.
Kwa kweli kauli ile ilinisikitisha sana kutokana na ukweli kwamba Asha
nilimchukulia kama dada yangu,kwani nilifanya naye kazi kwa miaka 14 iweje
hii leo aje anitolee maneno ya kunichafua katika vyombo vya habari?
Mimi sijawahi kuhusika na mpango wowote wa wasanii wa Twanga kuhamia
Mashujaa na wala sikuwa nafahamu mpango huo zaidi ya mwisho wa siku
kusikia fununu za chinichini na mwishowe wasanii hao kutangazwa kuhamia
Mashujaa.
Leo napenda nitangaze rasmi kwamba nimeachana na African Stars na
kujunga na Mashujaa Entertainment na tayari nimeshasaini mkataba wa kazi
katika bendi hii".
“Nilipanga nifanye taratibu za kumuaga kutokana na kuwa nilikuwa nafanya
kazi kwake bila ya mkataba lakini nimepata bendi hii ambayo tulikaa na
kukubaliana mambo mbalimbali.
Mbali na mkataba baadhi ya makubaliano na uongozi wa mashujaa ni pamoja
na kunipangia nyumba hali itakayoniladhimu kuhama ile iliyokuwa chini ya
Twanga.
Ninaamini nitafanya vema kazi yangu hii mpya kama ilivyokuwa Twanga
ambapo nilidumu kwa muda mrefu na kuchangia kufika hadi hapo nilipoachia,
hivyo naomba ushirikiano kwa uongozi, wanamuziki, Wadau na hata ninyi
mwaandishi wa habari."
Mwisho wa taarifa.

No comments:

Post a Comment