KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, May 24, 2012

Nimepata mpenzi wa kweli-Funke Akindele



LAGOS, Nigeria
MCHEZA filamu machachari wa Nigeria, Funke Akindele amesema anamshukuru Mungu kwamba kwa sasa amempata mpenzi wa kweli na anayempenda kwa dhati.
Akindele ameueleza mtandao wa naijerules wiki hii kuwa, kwa sasa yupo kwenye mapenzi mazito na haoni tatizo kukiri ukweli huo.
“Mimi si mtoto mdogo na naelewa nini maana ya kuwa katika mapenzi. Hili ni penzi la kweli. Nimempata nimpendaye,”alisema mcheza filamu huyo machachari wa Nollywood.
Alipoulizwa jina la mpenzi wake huyo, Akindele hakuwa tayari kulitaja. “Kuwa na furaha kwa ajili yangu, nimempata mpenzi wa kweli,”alisema.

No comments:

Post a Comment