KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Friday, May 11, 2012

Tafa Queens waahidiwa donge nono


MKE wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda ameahidi kuwazawadia wachezaji wa timu ya taifa ya netiboli, Taifa Queens sh. milioni moja kila mmoja iwapo watafanikiwa kubakisha nyumbani kombe la ubingwa wa Afrika.
Mama Tunu alitoa ahadi hiyo juzi wakati wa sherehe za ufunguzi wa michuano ya netiboli ya Afrika zilizofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Alisema kutokana na uchangishaji wa fedha za maandalizi kuvuka malengo, fedha zote zitakazobaki baada ya kumalizika kwa michuano hiyo watapatiwa wachezaji.
Mashindano hayo yanayozishirikisha nchi saba za Afrika, wakiwemo wenyeji Tanzania, yalifunguliwa rasmi na Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete.
Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Mama Salma alisema mashindano hayo yanapaswa kutumika kukuza ushirikiano miongoni mwa nchi za Afrika.
Mama Salma alitoa mwito kwa viongozi wa michezo na taasisi za mahusiano ya kimataifa katika nchi za Kiafrika, kutumia vizuri fursa za michezo katika kukuza na kuboresha mahusiano ya nchi zao.
Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara alivitaka vyama vya michezo kujipanga vizuri ili kuhakikisha vinafanikisha malengo yao .
Katika mechi ya ufunguzi iliyochezwa juzi, Taifa Queens ilianza vyema mashindano hayo baada ya kuichapa Lesotho mabao 57-13. Taifa Queens ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 40-13.



No comments:

Post a Comment