KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, May 30, 2012

Airtel yaongeza zawadi katika promosheni ya Nani Mkali

Ofisa Uhusiano wa Airtel, Dangio Kaniki akifafanua jambo wakati wa mkutano wa
waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi ya kushiriki promosheni ya Nani Mkali
iliyoongezwa muda andika neno “Mkali” tuma kwenda 15656 bure. Baada ya hapo
atatumiwa maswali na kila atakapo toa jibu sahihi atapata pointi 20 na jibu
lisilo sahihi pointi 10.Kila ujumbe wenye jibu utatozwa shillingi 350 pamoja na
kodi. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeongeza muda kwa
wateja wake kuendelea kucheza promosheni yake kabambe ya Nani mkali
ambayo ilianza miezi mitatu iliyopita na kuwafaidisha zaidi ya wateja 90 wa
Airtel waliojishindia jumla ya miliono 217 kwa mgawanyo wa kuanzia milioni
1 kila siku, milioni 3 kila wiki na milioni 30 kwa washindi wa mwezi
Akiongea na waandishi wa habari leo, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania,
Jackson Mmbando alisema promosheni hii imekuwa na faida kwetu Airtel
wateja wetu waliokuwa wakishiriki wameifurahia na ndio maana leo
tumeamua kuongeza zawadi na muda wa promosheni ya Nani Mkali.
Hivyo promosheni yetu inaongezwa muda wa miezi miwili huku zawadi
zitakazo toka ni pesa taslim Jumla ya ya shilingi milioni 143 katika mgawanyo
wa kuanzia shilingi milioni 1 kila siku-washindi 52, milioni 3 kila wiki
–washindi 7,na milioni 30 kwa kila mwezi itatoka kwa washindi 2.
Pia tutakuwa na washindi wengine watakaogawana kitita cha shilingi milioni
10 za zaidi ikiwa watakuwa kati ya wachezaji bora wa promosheni ya Nani
mkali
Ili mteja kushiriki na kujishindia zawadi hizi kabambe Afisa Mawasiliano wa
Airtel bi Dangio Kaniki alisema,” kudhihirisha kauli mbiu yetu ya jisikie huru
katika promosheni hii mteja anatakiwa kuandika neno “Mkali” na kutuma
kwenye namba 15656 bure kabisa ili kujiunga. Baada ya hapo atatumiwa
maswali na kila atakapo toa jibu sahihi atapata pointi 20 na jibu lisilo sahihi
pointi 10.Kila ujumbe wenye jibu utatozwa shillingi 350 pamoja na kodi.
Promosheni hii pia itatoa fursa kwa wateja kuchagua lugha wanayotaka kwa
kutuma neno “swa” kwa Kiswahili au “eng” kwa lugha ya kiingereza kwenda
namba 15595 Kujua alama ulizonazo au point mteja wetu atatakia kutuma
neno “point” au “alama” kupatiwa pointi alizojikusanyia. Kujiondoa kwenye
promosheni mteja atatakiwa kutuma neno “cancel’ au “stop” kwenda namba
15595
Promosheni ya nani mkali ilizinduliwa rasmi februari 15, 2012 na kudumu kwa
muda wa miezi mitatu.Nani Mkali imefanikiwa kuwazawadia wateja wa Airtel
kutoa mikoa mbali mbali ikiwemo Arusha, Muheza Tanga and DSM, Tabora,
Dodoma, Mwanza, Mbeya, Iringa, Kilimanjaroa na mingine mingi.

No comments:

Post a Comment