KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, May 24, 2012

D'Banj, Kanye West wacheza filamu ya ujambazi Qatar


LAGOS, Nigeria
MWANAMUZIKI nyota wa miondoko ya hip hop wa Nigeria, Dapo Oyebanji a.k.a D’Banj na mwanamuziki mwenzake wa miondoko hiyo wa Marekani, Kanye West wameshiriki kucheza filamu mpya.
Hata hivyo, filamu hiyo bado haijapewa jina, lakini inatarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni.
Picha za filamu hiyo, inayoelezewa kuwa ni ya aina yake, zimepigwa nchini Qatar na wanamuziki hao wamecheza nafasi ya ujambazi.
D’Banj wamekuwa wakitawala vyombo vya habari nchini Nigeria na Marekani kutokana na matukio mbalimbali. D’Banj hivi karibuni alitengana na bosi wake, Don Jazzy wakati Kanye ameripotiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Kim Kardashin.

No comments:

Post a Comment