KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, May 28, 2012

MISS SINZA KUANZA KUJINOA JUNI MOSI

MAZOEZI ya warembo wataowania taji la Miss Sinza 2012 yamepangwa kuanza Juni Mosi kwenye ukumbi wa Ten Star Lounge (Mawela Social Hall) ulipo karibu na hotel ya Vatican City uliopo Sinza.
Mratibu wa mashindano hayo, Majuto Omary(pichani) alisema kuwa mazoezi hayo yataanza saa 10.00 jioni na ni ya wazi kwa warembo wenye nia ya kutaka kuwania taji na zawadi nono za washindi wa mwaka huu ambao wataiwakilisha Sinza kwenye mashindano ya Kanda ya Kinondoni, Miss Tanzania na baadaye katika mashindano ya Dunia “Miss World”.
Majuto alisema kuwa fomu za washiriki zitatolewa hapo hapo kwenye ukumbi wa mazoezi na wengine wanaotaka kushiriki katika mashindano hayo wanatakiwa kufika ofisi za Mama Tike Hair Fashion and Boutique zilizopo Sinza Kumekucha kituoni, Ofisi za Miss Tanzania (Posta), ofisi za SMP zilizopo Kinondoni Mkwajuni, Brake Point (Kijitonyama na Posta) na kupitia mtandao wa balilemajuto.blogspot.com, sufiani mafoto.blogspot.com.
Alisema kuwa kamati ya Miss Sinza kwa sasa ipo katika mikakati mbali mbali ya kusaka wadhamini kwa ajili ya kufanikisha mashindano hayo yanayotarajiwa kuwa bora kabisa mwaka huu.
“Tunaomba wadhamini ikiwa ni makampuni, wafanya biashara, wadau wa masuala ya urembo ambao wanataka kujitangaza kupitia mashindano haya kujitokeza kusaidia waandaaji kwani lengo kubwa ni kuona Sinza inafanya mashindano bora na yenye kuleta mafanikio makubwa kwa kutwaa taji la Miss Tanzania na lile la Dunia,” alisema Majuto.
Alifafanua kuwa wameandaa mikakati na mipango mbali mbali ili kuhakikisha Sinza mwaka huu inapata mafanikio makubwa katika mashindano ya Miss Tanzania na yale ya Dunia.

No comments:

Post a Comment