KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, May 28, 2012

MISS DAR INTER COLLEGE JUNI *

SHINDANO la kumsaka Miss Dar Intercollege 2012 linatarajiwa kufanyika Juni
8 kwenye ukumbi wa Sunciro, ulipo Sinza Shekilango jijini Dar es Salaam,
imefahamika.
Mratibu wa Shindano hilo Dina Ismail alisema jana kwamba warembo
watakaoshiriki shindano hilo wanaendeleza na mazoezi kwenye hoteli ya
Lamada jijini Dar es Salaam chini ya ukufunzi wa Marylidya Boniface, huku
kwa upande wa shoo wakinolewa na Bob Rich.

Alisema mpaka sasa warembo 12 kutoka vyuo vya Biashara (CBE), Uandishi
wa Habari (DSJ) na Time, Ustawi wa Jamii na kile cha Usimamizi wa Fedha
(IFM) wamesharipoti kambini.

Dina aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Hilda Edward, Nancy
Maganga, Saada Seleman, Neema Nashon, Rose Muchunguzi, Fina
Revocatus,Jane Augustino,Theresia Issaya na Natasha Deo.

Taji la kitongoji hicho linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM.

Kwa upande mwingine, mratibu huyo ameyaomba makampuni mbalimbali
kujitokeza kudhamini shindano hilo ambalo linatarajiwa kuwa la aina yake na
hasa ikizingatiwa kuwa washiriki wake wana vigezo vya hali ya juu.

“Tunaomba makampuni mbalimbali yajitokeze kudhamini shindano
letu. Mpaka sasa wadhamini tulionao ni pamoja na kampuni ya Bia Tanzania
(TBL) kupitia bia ya Redd’s, Lamada Hotel, Ndege Insurance, Dodoma Wine na
Clouds Fm.

No comments:

Post a Comment