KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, May 24, 2012

Uche Jombo avunja ukimya

LAGOS, Nigeria
HATIMAYE mcheza filamu wa kike mwenye mvuto nchini Nigeria, Uche Jombo amethibitisha kufunga ndoa hivi karibuni nchini Venezuela.
Uche ameamua kuvunja ukimya huo baada ya vyombo kadhaa vya habari nchini Nigeria kuripoti wiki iliyopita kwamba, amefunga ndoa kwa siri.
Mwanadada huyo aliripotiwa kufunga ndoa na mpenzi wake wa Kimarekani.
“Ndio ni kweli, lakini siwezi kutoa taarifa zingine zaidi kwa sasa. Lakini naahidi kufanya hivyo hivi karibuni,”alisema Uche.
Kwa mujibu wa Uche, walifunga ndoa hiyo Mei 16 mwaka huu katika mji wa Puerto Rico na kuhudhuriwa na watu kadhaa maarufu, akiwepo rafiki yake wa karibu, Desmond Elliot.

No comments:

Post a Comment