KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, May 29, 2012

Airtel yakabidhi vifaa vya michezo kwa DRFA

Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania,Jane Matinde akisisitiza jambo wakati
akiongea na waandishi wa habari (hawako pichani) wakati wa kukabidhi vifaa
vya michezo kwa timu za shule za sekondari zitakazoshiriki michuano ya Airtel
Rising Stars ambayo inatarajiwa kuanza kesho,jumatano Mei 30.



Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania,Jane Matinde akimkabidhi jezi Katibu Mkuu wa
chama cha mpira mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) wakati kampuni ilipokabidhi
vifaa vya michezo kwa timu za shule za sekondari zitakazoshiriki michuano ya
Airtel Rising Stars ambayo inatarajiwa kuanza kuanza kesho,Jumatano Mei 30.



Airtel Tanzania jana ilikabidhi vifaa vya michezo kwa timu za shule za
sekondari 24 zitakazoshiriki kwenye michuano ya vijana wenye umri chini ya
miaka 17 maarufu kama Airtel Rising Stars ambayo inatarajiwa kuanza
kutimua vumbi kesho Mei 30, ngazi ya Mkoa.
Shule zitakazoshiriki kwenye michuano hiyo ni zile zilizofanya vyema kwenye
michuano ya shule za sekondari (UMISSETA), ambazo ni Lindi sekondari,
Mpunyule na Nkowe zote za Mkoa wa Lindi, Southern Highland, Mbeya Day na
Wenda Sekondari kutoka Mbeya.
Nyingine ni Mbande Sekondari, Kurasini na Kiravi (Temeke), Airwing,
Benjamini Mkapa na Msogola Sekondari (Ilala), Twiga Sekondari, Goba na
Makongo Sekondari (Kinondoni), Sinoni, Kaloleni na Bishop Durning (Arusha).
Timu hizo zote zimethibitisha ushiriki wao na kuahidi kufanya vizuri ili
kushinda mechi zao. Mechi za mikoa zitatumika kuchangua timu kombaini
zitakazowakilisha mikoa kwenye mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya
taifa yatakayoanza Juni 9 mpaka Juni 17 Jijini Dar es Salaam.
Wakati timu za wavulana zikatarajiwa kushindana kwenye ngazi ya mkoa ili
kuchanguliwa kucheza michuano ya Taifa, timu moja kutoka kila Mkoa itafuzu
moja kwa moja na kufanya timu zitakazoshiriki ngazi ya taifa kuwa 12, sita za
wavulana na sita wasichana.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar
es Salaam leo, Meneja Masoko na Matangazo Airtel Tanzania Rahma
Mwapachu alisema Airtel inajivunia ushirika wake na moja ya Klabu kubwa
duniani - Machester United, kuinua kiwango cha mpira wa miguu nchini
Tanzania na Afrika.
'Tunaamini ya kuwa kwa ushirikiano wetu na Manchester United na TFF
tutakuza kwa kiasi kikubwa kiwango cha mpira wa miguu hapa nchini
Tanzania. Tunaamini vijana wakiandaliwa vizuri wanaweza'.Mwapachu
alishukuru Wizara ya Habari, Vijana, Utamanduni na Michezo kwa ushirikiano
wanaotoa ili kukuza mpira hapa nchini.
Airtel Rising Stars ni mpango kabambe wa Afrika nzima ambao ni kuibua na
kukuza vipaji vya wanasoka wanaochipukia, wavulana na wasichana wenye
umri wa miaka chini ya kumi na saba ambao watapata muda muafaka wa
kuonyesha vipaji vyao na kukutana na waatalum wa mpira wa miguu na
kupata mafunzo zaidi hivyo kukuza vipaji vyao.
Mwaka jana, Klabu ya Manchester United ilitoa walimu wake wa soka la vijana
kufundisha kliniki za soka za kimataifa zilizofanyika Tanzania, Afrika Kusini na
Gabon ambapo walishiriki walipata nafasi ya kufundisha jinsi ya kucheza mpira
wa miguu kwa mtindo wa Manchester United.
Kliniki ya aina hiyo itafanyika Jijini Nairobi Agosti mwaka huu kwa nchi
zinazozungumza Kingereza Tanzania ikiwemo. Nairobi pia itakuwa mwenyeji
wa mashindano ya Airtel Rising Stars inter-continental ambayo itashirikisha
nchi 14 ambapo Airtel inafanya biashara. Tanzania itawakilishwa na mshindi
wa fainali za taifa pamoja na wachezaji sita bora, watatu wavulana na watatu
wasichana.

No comments:

Post a Comment