KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, May 28, 2012

Twiga Stars yachapwa mabao 2-1

TIMU ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars, imeanza vibaya kampeni za kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa kwa wanawake, baada ya kufungwa mabao 2-1 jioni hii mjini Addis Ababa na wenyeji, Ethiopia.

Twiga sasa inahitaji ushindi wa 1-0, Juni 16, katika mchezo wa marudiano mjini Dar es Salaam, ili kukata tiketi ya kucheza fainali hizo kwa mara ya pili mfululizo, Novemba mwaka huu, Equatorial Guinea, zikiwa ni za nane katika historia ya michuano hiyo

No comments:

Post a Comment