KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, May 24, 2012

FLAVIANA MATATA AKUMBUKA MBALI

Mwanamitindo maarufu wa Tanzania, Flaviana Matata akibubujikwa na machozi wakati wa ibada ya kuwakumbuka watu waliofariki katika ajali ya meli ya MV Bukoba iliyotokea miaka 16 iliyopita kwenye Ziwa Victoria. Ibada hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye makaburi ya Igoma mjini Mwanza. Mrembo huyo, ambaye alimpoteza mama yake kutokana na ajali hiyo, alitoa misaada ya vifaa mbalimbali vya kujikinga na ajali.

No comments:

Post a Comment