KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, May 28, 2012

Airtel Jiunge na Supa 5 yapasua anga mkoani Dodoma

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto) akikabidhi
zawadi ya simu kwa, Baltazar Theobald, mshindi wa kwanza aliyeweza kueleza
vizuri jinsi ya kujiunga na huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa 5 wakati wa
hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki. Airtel
Jiunge na Supa 5 Ilizinduliwa kwa mara ya kwanza jijini Dar es Salaam hivi
karibuni.


Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wa kundi la Wanaume Family, Said
Juma ‘Chege’ (kushoto) na Amani James Temba ‘Mheshimiwa
Temba’wakionyesha makali yao katika onyesho la uzinduzi wa huduma ya
Airtel Jiunge na Supa 5 mjini Dodoma mwishoni mwa wiki



Mpiga tumba mahiri wa bendi ya Mashujaa Musica aliyejiunga na bendi hiyo akitokea
Twanga Pepeta, Sudi Mohamed ‘MCD’ akionyesha makali yake wakati wa
onyesho la uzinduzi wa huduma ya Airtel Jiunge na Supa 5 mjini Dodoma
mwishoni mwa wiki.



Rais wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel Cyprian ‘ Chaz Baba’ ambaye naye amehama akitokea Twanga Pepeta, akiimba wakati wa onyesho la uzinduzi wa huduma ya Airtel Jiunge na Supa 5 mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.



Msanii wa kundi la muziki wa bongo fleva la Tip Top Connection lenye maskani yake mitaa ya Manzese jijini Dar es Salaam Hamad Ally ‘Madee’ akichengua mashabiki wake waliojitokeza katika onyesho la uzinduzi wa huduma ya Airtel Jiunge na Supa 5 mjini Dodoma mwishoni
mwa wiki.


Huduma ya SUPA 5 imepokelewa kwa shangwe mkoani Dodoma huku
dhamira yake ikiendelea kutimia baada ya umati mkubwa wa vijana kujitokeza
ili kufahamu vyema huduma hiyo nafuu iliyozinduliwa wiki moja iliypota kwa
lengo la kuwapa unafuu wateja wa Airtel ili kufurahia huduma tano nafuu
Wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika tamasha la wazi katika viwanja vya
Barafu mjini Dodoma wasanii wa muziki wa Dansi na Bongo Flaver
walitumbuiza na kufanya tamasha hilo kufana zaidi
Miongoni mwa wasanii waliotumbuiza kwenye utambilisho wa huduma hiyo
mpya kabambe ni pamoja na bendi ya muziki ya mashujaa, kundi la muziki
wa kizazi kipya la Tiptop Connection na kundi la Wanaume TMK.
Akitambilisha huduma hiyo mbele ya wakazi wa mji wa Dodoma na vitongoji
vyake Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando amesema, wateja wa
kampuni hiyo watapata unafuu mkubwa wa gharama za kupiga simu
“Huduma ya SUPA 5 inamuwezesha mteja wa Airtel kutumia mtandao wa
facebook bure masaa 24, kuongea nusu shilingi na watu watatu, kupiga simu
kwa robo shilingi kuanzia saa 4 usiku hadi saa 12 asubuhi na kutumia huduma
ya internet bure usiku kucha” alieleza Bw, Mmbando
Huduma ya SUPA 5 itaendelewa kutambulishwa katika mikoa mbali mbali kwa
kuwa huduma hiyo nafuu ni ya kudumu, mikoa inayotarajiwa kutembelewa
kwa kufanyiwa utambulisho rasmi wa huduma hiyo ya Airtel Supa 5 ni pamoja
na Morogoro, Iringa, Arusha, Mwanza na DSM.

No comments:

Post a Comment