KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, September 11, 2016

AJIB, MAVUGO WALETA RAHA SIMBA


MABAO yaliyofungwa na washambuliaji Ibrahim Ajib na Laudit Mavugo jana yaliiwezesha Simba kuibuka na mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, katika mechi ya ligi kuu ya Tanzania Bara, iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Kutokana na ushindi huo, Simba sasa imeungana na Azam kushikilia usukani wa ligi hiyo, ambapo timu zote mbili zina pointi 10 kila moja baada ya kucheza mechi nne, huku zikilingana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.

Ajib alifunga bao la kwanza dakika ya 52 kwa kichwa akimalizia kona nzuri iliyochongwa na beki Mohammed Hussein 'Tshabalala'.

Mavugo aliongeza bao la pili dakika ya 66 akiwa ndani ya boksi baada ya pasi ya kiungo Mwinyi Kazimoto.

No comments:

Post a Comment