KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Saturday, September 7, 2013

SIMBA YAICHEZESHA KWATA KMKM



HABARI NA ZAITUN KIBWANA, PICHA NA BIN ZUBEIRY BLOG
SIMBA SC imeendelea kung’ara katika michezo ya kirafiki baada ya jioni hii kuilaza timu ya Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM) ya Zanzibar mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mabao ya Simba katika mchezo huo ulioanza saa 11:05 jioni yalifungwa na beki Mrundi, Kaze Gilbet na kiungo mzalendo Said Ndemla.  Hadi mapumziko, tayari Wekundu wa Msimbazi walikuwa mbele kwa mabao 2-0.

Simba ilipata bao lake la kwanza dakika ya 28 baada ya Ndemla kupokea pasi ya Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ upande wa kushoto na kuingia ndani akiwachambua mabeki kabla ya kumtungua na kipa wao, Mudathir Khamisi aliyevutika.
Simba ikapata bao la pili dakika ya 41 kwa shuti la moja kwa moja la mpira wa adhabu lililopigwa na beki Gilbert, kufuatia Ramadhani Chombo ‘Redondo’ kuchezewa rafu.
Pamoja na kufungwa mabao hayo ya kipindi cha kwanza, lakini KMKM iliyoongozwa na wachezaji wenye uzoefu na soka ya Bara, kiungo Abdi Kassim ‘Babbi’ aliyewahi kucheza Mtibwa Sugar, Yanga SC na Azam na Ally Ahmed ‘Shiboli’ aliyecheza Simba SC, Kagera Sugar na Coastal Union iliendelea kucheza vizuri.  
 
KMKM inayofundishwa na kipa wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Ally ‘Bush’ Bushiri ilipata bao lake dakika ya 54 kupitia kwa Iddi Kambi aliyewazidi ujanja mabeki wa Simba SC inayofundishwa na mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’.

Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Andrew Ntalla, Haruna Shamte, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Hassan Hatibu, Kaze Gilbert, Abdulhalim Humud, Twaha Ibrahim, Said Ndemla, Amisi Tambwe, Ramadhani Chombo ‘Redondo’/Betram Mombeki na Zahor Pazi.
KMKM; Mudathir Khamis, Kassim Nemshi, Faki Hamad, Iddi Mgeni, Khamis Ali, Ibrahim Khamis, Nassor Ali, Abdi Kassim ‘Babbi’, Ally Ahmed ‘Shiboli’, Mwinyi Ameir na Iddi Kambi. 

No comments:

Post a Comment