KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, September 4, 2013

SIMBA YAWAONYA WANAOUZA JEZI ZAO



KLABU  ya Simba imewataka wafanyabiashara wanaotumia nembo ya klabu hiyo bila kuwa na kibali, kujisalimisha kwa uongozi haraka iwezekanavyo.

Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema mjini Dar es Salaam jana kuwa, wasiofanya hivyo, watachukuliwa hatua za kisheria.

"Kuanzia Jumatatu, kutakuwa na msako mkali ili kuwakamata wale wote wanaofanya biashara ya bidhaa zenye nembo ya Simba bila ya kuwa na kibali,"alisema.

Kamwaga alisema tabia hiyo imekuwa ikiikosesha mapato klabu hiyo kutokana na ukweli kwamba, watu waliopewa mamlaka ya kuendesha biashara kwa kutumia nembo hizo, wameshindwa kuiendesha kutokana na watu wengine kuzalisha bidhaa zenye viwango vya chini.

"Sisi tumetoa kibali kwa wafanyabiashara wawili tu, ambao wanauza bidhaa orijino, mfano jezi moja sh 25,000, lakini kuna watu wanatengeza jezi hafifu na kuuza kwa sh 7,000 na watu wengi wanazinunua hizo na kuikosesdha klabu mapato,"aliongeza Kamwaga.

Katika hatua nyingine, klabu hiyo imezindua anuani maalum ya barua pepe kwa ajili ya wadau na wanachama kutoa mapendekezo yao ambayo wanahitaji yawemo kwenye katiba ya klabu hiyo.

Ameitaja anuani hiyo kuwa ni:  maoniyakatibayasimba@yahoo.com. Maoni hayo
yatapokelewa hadi Septemba 20 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment