KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Saturday, September 14, 2013

ILALA KUCHEZA FAINALI NA MJINI MAGHARIBI




Ilala imepata tiketi ya kucheza fainali ya michuano ya Copa Coca-Cola kwa vijana wenye umri chini ya miaka 15 upande wa wavulana baada ya kuivua ubingwa Morogoro katika mechi iliyoamriwa kwa mikwaju ya penalti.

Hadi muda wa kawaida wa mchezo huo uliochezwa leo (Septemba 13 mwaka huu) jioni Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, jijini Dar es Salaam timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1.

Paul Ngowi ndiye aliyeanza kuifungia Ilala dakika ya 30, lakini Morogoro wakasawazisha dakika ya 50 kupitia kwa Omari Sultan. Katika changamoto ya mikwaju ya penalti, Ilala ilipata tatu dhidi ya mbili za Morogoro.

Ilala sasa itacheza fainali na Mjini Magharibi itakayofanyika kesho (Septemba 14 mwaka huu) kuanzia saa 9 alasiri.

Fainali hiyo ya wavulana itatanguliwa na ile ya wasichana kati ya Mwanza na Ilala itakayoanza saa 7 mchana. Mwanza imepata tiketi ya kucheza fainali baada ya leo kushinda nusu fainali ya pili dhidi ya Mbeya kwa mabao 3-0.

Mabao hayo katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume yamefungwa na Flora Fulgence dakika ya 47, Emiliana Akuti dakika ya 56 na Yulitha Masamu dakika ya 57.
AIRTEL RISING STARS KUKABIDHIWA BENDERA
Timu ya Airtel Rising Stars ya Tanzania kwa wavulana na wasichana itakabidhiwa bendera kesho (Septemba 14 mwaka huu) tayari kwa safari ya Nigeria itakayofanyika keshokutwa alfajiri.

Hafla hiyo ya kukabidhi bendera kwa timu hiyo yenye kikosi cha wachezaji 32 itafanyika saa 5 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah ndiye atakayekabidhi bendera kwa kikosi hicho.

No comments:

Post a Comment