KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, September 2, 2013

HENRY JOSEPH AITWA TAIFA STARS



Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amemjumuisha mchezaji Henry Joseph wa
Simba kwenye kikosi chake kinachojiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia
dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul.

Tayari Joseph amesharipoti kwenye kambi ya timu hiyo iliyoko hoteli ya Accomondia
jijini Dar es Salaam.

Taifa Stars ambayo iko chini ya udhamini wa Kilimanjaro
Premium Lager imeingia kambini tangu Agosti 29 mwaka huu, na leo jioni itafanya
mazoezi yake kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.

Programu ya timu hiyo inaonesha kuwa kesho (Septemba 3 mwaka huu) itafanya
mazoezi yake asubuhi na jioni kwenye uwanja huo huo wa Kumbukumbu ya
Karume.

Wakati huo huo, kesho (Septemba 3 mwaka huu) saa 6 kamili mchana Kocha Kim
Poulsen atakuwa na Mkutano na Waandishi wa Habari.

LIUNDA KUTATHMINI WAAMUZI CL
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Leslie Liunda wa Tanzania kuwa
mtathmini wa waamuzi kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Coton Sport
ya Cameroon na Esperance ya Tunisia.

Mechi hiyo ya kundi B itachezwa Septemba 21 mwaka huu kwenye Uwanja wa
Omnisport Roumdeadjia mjini Garoua, Cameroon. Kamishna atakuwa Bema
Doumbia wa Ivory Coast.

Waamuzi wanatoka Madagascar wakiongozwa na Hamada Nampiandraza. Wasaidizi
wake ni Jean Eric Pierre Andrivoavonjy, Ferdinand Velomanana Linoro na Bruno Marie
Andrimiharisia.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

No comments:

Post a Comment