Hoteli ya Serengeti Golden Paradise Resort imeleta mapinduzi makubwa katika kutoa huduma za hoteli na burudani ya muziki katika maeneo ya Mbande, Mbagala, ambayo yako pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam.
Licha
ya ukumbi wa hoteli hiyo kuwa wa kisasa na wenye uwezo wa kuchukua mashabiki
wengi kwa wakati mmoja, unaweza kuonekana mdogo kutokana na kujitokeza kwa
umati mkubwa wa watu wakati wa maonyesho mbalimbali.
Meneja
wa hoteli hiyo, Wambura Sungura anasema
kuzinduliwa kwa ukumbi huo kumeleta faraja kubwa kwa wakazi wa Mbagala na
vitongoji vyake kutokana na kupata huduma, ambazo wamekuwa wakizikosa na badala
yake kulazimika kusafiri kwenda mbali kuzitafuta.
“Kwa
sasa ni kama kuunga mkono mpango wa serikali wa kuhakikisha huduma zote muhimu
kama hizi za hoteli zinapatikana nje ya miji ili kupunguza kila kitu watu
wakifate mjini, matokeo yake kusababisha msongamano mjini bila sababu za
msingi,”anasema.
“Pia
siku hizi watu hawataki bugudha mijini, badala yake wanataka kwenda sehemu
tulivu na zenye hadhi kama hizi kwa kupumzika baada ya shughuli za wiki nzima,
hali inayowafanya watafute sehemu nzuri za kupumzika na sehemu za namna hii ni
nzuri kwao,”anasema Sungura.Meneja huyo anasema wameandaa utaratibu wa kuvialika vikundi mbalimbali vya burudani kila mwisho wa wiki ili kutoa fursa kwa wakazi wa Mbagala na vitongoji vyake kutohangaika kusafiri umbali mrefu kwenda mjini au maeneo mengine kutafuta burudani.
“Tunataka watu wasiwe wanahangaika kutoka hapa kutafuta burudani, tutajitahidi kuhakikisha kuwa kila wasanii wanaopendwa na wateja tunawaleta ili kukoga nyoyo zao,”anasema.
Anaongeza
kuwa, kwa sasa wanatoa huduma mbalimbali ikiwemo malazi, vinywaji na chakula,
kitu ambacho kama mteja akifika hapo
hawezi kujutia nafsi yake, badala yake atakuwa anatamani kwenda kupata huduma
mara kwa mara.
Anasema
pamoja na kufungua hoteli hiyo, wanashiriana na wateja kupata maoni yao juu ya
namna bora ya kuboresha huduma ili kuleta mageuzi makubwa katika kutoa huduma
bora zaidi.
No comments:
Post a Comment