KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Saturday, March 1, 2014

TWIGA STARS YATUPWA NJE NA ZAMBIA KOMBE LA AFRIKA



TIMU ya soka ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars imetolewa katika hatua za awali za michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Zambia katika mchezo wa marudiano wa raundi ya kwanza uliochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.


Matokeo hayo yanaifanya Zambia, Shepolopolo isonge mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2, kufuatia awali kushinda 2-1 nyumbani katika mchezo wa kwanza.

Twiga inayofundishwa na Rogasian Kaijage, iliuanza vizuri mchezo wa leo na kumaliza dakika 45 za kipindi cha kwanza ikiwa inaongoza bao 1-0, lililofungwa na Asha Rashid ‘Mwalala’ dakika ya 39.

Asha Mwalala alifunga bao hilo akimalizia pasi ya Vumilia Maarifa, ambaye naye alipokea krosi ya Nahodha Sophia Mwasikili aliyewachambua wachezaji wa Zambia.

Kipa wa Twiga Stars, Fatuma Omary aliokoa mchomo wa hatari wa Mupopo Kabange dakika ya 75, lakini hakuweza kuuona mkwaju wa mpira wa adhabu uliopigwa na Rachel Ilungu dakika ya 80 kuipatia Zambia bao la kusawazisha.

Twiga Stars: Fatuma Omary, Fatma Bashir, Deonisia Daniel, Fatma Issa, Evellyne Sekikubo, Sophia Mwasikili, Vumilia Maarifa, Amina Ali/Zena Khamis dk86, Asha Rashid, Shelda Boniface/Fatma Mustapha dk 65 na Eto Mlenzi.

No comments:

Post a Comment