KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, March 5, 2014

NGASA AMZIMIA TAMBWE




MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Yanga, Mrisho Ngasa, amesema anavutiwa na staili ya uchezaji na uhodari wa kufunga mabao wa mshambuliaji Hamisi Tambwe wa Simba.

Ngasa alisema hayo wiki hii kupitia akaunti yake ya Twitter, ikiwa ni siku moja baada ya Simba kuichapa Ruvu Shooting mabao 3-2 katika mechi ya ligi kuu ya Tanzania Bara, iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mechi hiyo, Tambwe aliifungia Simba mabao mawili kati ya matatu na kumfanya aweke rekodi ya kufunga mabao 19 katika ligi hiyo hadi sasa.

Ngasa amemwelezea Tambwe kuwa ni mshambuliaji bora na mwenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao kuliko washambuliaji wa timu zingine zinazoshiriki katika ligi hiyo.

"Siku zote huwa napenda kusema kwenye ukweli ni vyema tu kusema, Tambwe ni mshambuliaji," ameandika Ngasa kwenye mtandao huo.

Katika hatua nyingine, Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic amekiri kuwa, uwezo wa Tambwe katika kufunga mabao ni wa kiwango cha juu na amewataka wachezaji wengine kuiga mfano wake.

Loga alisema mjini Dar es Salaam wiki hii kuwa, tangu alipoanza kibarua cha kuinoa Simba, amegundua kwamba Tambwe ni mchezaji anayejituma na hiyo ndiyo siri kubwa ya mafanikio yake.

"Tambwe anapenda sana mazoezi na ni msikivu kwa kocha. Anafanya kile unachomuelekeza kukifanya,"alisema kocha huyo kutoka Serbia.

No comments:

Post a Comment