
Matokeo hayo yaliiwezesha Twiga Stars kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 7-2, kufuatia kuichapa Namibia mabao 2-0 katika mechi ya awali iliyochezwa mjini Whindhoek.
Mshambuliaji Mwanahamisi Omary ndiye aliyeibuka shujaa wa Twiga Stars baada ya kuifungia mabao matatu kati ya matano. Mwanahamisi alizawadiwa pesa nyingi na mashabiki.
Twiga Stars sasa itakutana na mshindi kati ya Misri na Ethiopia, ambazo zilitarajiwa kurudiana jana mjini Addis, Ababa. Katika mechi ya awali, Misri ilishinda mabao 4-2.
No comments:
Post a Comment