KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, January 12, 2012

Uche Jombo apigwa kibuti

Uche Jombo

Uche Ikechukwu


LAGOS, Nigeria
MWIGIZAJI mwenye makeke wa Nollywood, Uche Jombo amepigwa kibuti na mpenzi wake wa muda mrefu, mwanasoka wa kimataifa wa Nigeria, Uche Ikechukwu.
Imedaiwa kuwa, Ikechukwu ameamua kumpiga kibuti mwanadada huyo baada ya kumweleza kuwa, hakuwa katika penzi la dhati na yeye.
Habari kutoka kwa watu wa karibu na mwanasoka huyo zimeeleza kuwa, siku zote hakuwa muwazi kuhusu penzi lake na mcheza filamu huyo.
Miezi kadhaa iliyopita, kulikuwa na habari kuwa wapenzi hao wawili walikuwa wakifanya mipango ya kufunga ndoa ili kuwa mume na mke.
Vyanzo vya habari vimeeleza kuwa, Ikechukwu alikuwa amemvisha Uche Jombo pete ya uchumba iliyotengenezwa kwa vito vya almasi.
Imedaiwa kuwa, mara baada ya kuvishwa pete hiyo, mwanadada huyo alikuwa akipenda kuionyesha kwa rafiki zake huku akiwa na uhakika mkubwa wa ndoa.
Vyanzo hivyo vya habari vimeeleza kuwa, uhusiano kati ya wapenzi hao wawili sasa umekufa na Uche Jombo havai tena pete ya uchumba aliyopewa na Ikechukwu.
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, uamuzi huo wa Ikechukwu umemchanganya akili Uche Jombo, ambaye kwa sasa hataki kabisa kuzungumzia suala hilo.
Mmoja wa marafiki wa Ikuchukwu alisema: ”Ikechukwu alikuwa kama mtu anayejifurahisha, hakuwa na lengo la kumuoa Uche Jombo. Japokuwa baadhi ya wakati alikuwa akionekana kama amepagawa kwa penzi la Uche Jombo, lakini hana mpango naye. Anayo mipango mingine kabisa ya baadaye.
Hivi karibuni, Ikechukwu alionekana akiwa kwenye klabu moja ya usiku na kaka yake, Kalu huku wakiwa na wasichana.

No comments:

Post a Comment