KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, January 12, 2012

Nyota wa Nollywood abakwa



LAGOS, Nigeria

MCHEZA filamu nyota wa kike nchini Nigeria (jina linahifadhiwa) hivi karibuni alibakwa na wasanii wenzake baada ya kulewa chakari.
Binti huyo mantashau alikutwa na masaibu hayo chumbani kwake kwenye hoteli aliyofikia baada ya kujibwaga kitandani na kusahau kufunga mlango.
Mcheza filamu huyo, aliyeolewa na kuachika mara kadhaa, alikuwa amelewa chakari baada ya kufakamia pombe kupita kiasi katika hafla iliyofanyika katika mji wa Asaba uliopo katika jimbo la Delta.
Alikuwa amekwenda Asaba akitokea Lagos kwa ajili ya kushiriki kucheza filamu mpya, akiwa na waigizaji wenzake kadhaa wa Nollywood.
Mara baada ya kumalizika kwa kazi hiyo siku ya kwanza, binti huyo alijumuika na wasanii wenzake kwa ajili ya vinywaji kwenye hoteli aliyofikia.
Mbali na kunywa pombe kupita kiasi, imeelezwa kuwa mcheza filamu huyo alivuta sigara nyingi, ikiwa ni kawaida yake kila anapopata kilevi.
Burudani hiyo ya vinywaji iliyokolezwa na muziki, ilimfanya mwanadada huyo achangamke na kuzidi kufakamia pombe, utadhani hakuwa akielewa madhara yake.
Hata hivyo, mwanadada huyo aliweza kumudu kurejea hadi chumbani kwake, ambako alijibwaga moja kwa moja kitandani bila kukumbuka kufunga mlango kwa funguo.
Mmoja wa waigizaji wa kiume, ambaye naye alikuwa amepanga hotelini humo, wakati akielekea chumbani kwake, alikosea na kufungua chumba cha mwanadada huyo.
Alichokishuhudia humo chumbani ni kumuona mwanadada huyo akiwa amejilaza kitandani akiwa kama alivyozaliwa, hali iliyomfanya ashindwe kujizuia.
Alichokifanya ni kufunga mlango wa chumba hicho na kuanza kumwingilia mwanadada huyo, ambaye muda wote wa kitendo hicho, hakuweza kujitambua.
Baada ya kuridhika na burudani aliyoipata, kijana huyo aliondoka chumbani humo na ndipo yule mwanadada alipozinduka na kugundua kwamba alikuwa ameliwa uroda na mtu asiyejulikana huku mlango wa chumba chake ukiwa wazi.
Imedaiwa kuwa, mwigizaji aliyemla uroda mwanadada huyo amekuwa akitamba na kujisifu kwa vile hakutarajia katika maisha yake kuweza kumnasa binti mzuri wa aina ile.

No comments:

Post a Comment