KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, January 26, 2012

SAUTI ZA BUSARA; Ni siku nne za shangwe za muziki wa Kiafrika



Baada ya kupokea maombi zaidi ya 560 kutoka vikundi mbalimbali ambavyo vinataka kufanya maonyesho yao katika tamasha la tisa la Sauti za Busara, hatimaye vikundi 31 vimechaguliwa kufanya maonyesho katika tamasha la tisa la sauti za busara ambalo limepangwa kufanyika kuanzia tarehe 8 mpaka 12 Februari katika ukumbi wa kihistoria wa Ngome Kongwe, Zanzibar.
Orodha ya wasanii imejumuisha wasanii mashuhuri kutoka Afrika Mashariki, Nigeria, Sudan,Cape Verde, Afrika Kusini, Kongo Brazaville,Comoro, Madagaska na kutoka Visiwa vya ushelisheli. Wasanii watakaopanda jukwaani ni Nneka (Nigeria),Tumi&The Volume (South Africa), Fredy Massamba(Congo), FM Academia (Tanzania) na Super Mazembe (Kenya).
Matukio mbalimbali ya ziada ya busara yataanza jumatano ya tarehe 8, milango itafunguliwa kwa matukio mbalimbali. Mji mkongwe utakuwa na maonyesho ya vikundi mbalimbali kama Nadi Ikhwan Safaa (aka Malindi Taarab), Maulidi ya Homu ya Mtendeni,Black Roots, Culture Musical Club na wengineo wengi.
Tamasha litafunguliwa na maandamano ya aina yake siku ya Alhamisi tarehe 9 Februari 2012 ambayo yataanzia katika viwanja vya Kisonge (Michenzani). Vikundi vitakavyoshiriki ikiwemo Kozman Ti Dalon,beni brass, kikundi cha wanawake cha mwanandege,wacheza kapoera na sarakasi, maandamano yatazunguka katika baadhi ya mitaa na kumalizikia Mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome Kongwe kwa ufunguzi rasmi wa tamasha la tisa.
Siku ya kwanza ya ufunguzi itapambwa na burudani kutoka kwa vikundi vifuatavyo Swahili Vibes, Shirikisho Sanaa,Tandaa Traditional group, Wanafunzi wa SOS (vyote kutoka Zanzibar), Mkota Ngoma kutoka Pemba na Ary Morais kutoka Cape Verde.
Siku ya pili tarehe 10 ijumaa, itapambwa na mkongwe wa taarab mwenye historia Afrika mashariki Bi Kidude kutoka Zanzibar na Ogoya Nengo kutoka Kenya. Wasanii wengine ambao watafanya onyesho siku hiyo ni Hanitra (Madagascar), Camirata Group (Sudan), Tausi Women’s Taarab na Utamaduni JKU (Zanzibar), Kozman Ti Dalon (Reunion), Fredy Massamba (Congo) na Super Mazembe (Kenya).
Jumamosi kutakuwa na mpambano wa vikundi vya mchiriku kutoka katika mitaa ya Dar es Salaam,Tanzania,Seven survivor na Jagwa Music, vikitanguliwa na Tunaweza Band (Tanzania), Ndere Troupe (Uganda), Jembe Culture Group (Tanzania), Camirata Group (Sudan) pamoja na Nneka,mwanadada kutoka Nigeria na mshindi wa tuzo ya MOBO ya mwaka 2009 ya mwanamuziki bora wa Afrika.
Jumapili tarehe 12 tutatumbuizwa na Qwela (Uganda), Leo Mkanyia (Tanzania), Lumumba Theatre Group (Tanzania), Chebli Msaidie (Comoros), Kidumbaki JKU (Zanzibar), Tumi & The Volume (South Africa) na FM Academia (Tanzania).
Siku ya jumapili ya tarehe 12, siku ya mwisho ya tamasha, tamasha litafungwa Qwela (Uganda), Leo Mkanyia (Tanzania), Lumumba Theatre Group (Tanzania), Chebli Msaidie (Comoros), Kidumbaki JKU (Zanzibar), Tumi & The Volume (South Africa) na FM Academia (Tanzania).
Kutakuwa na maonyesho ya filamu za muziki wa taarab, hiphop, kuduro na bongo flava,ambazo zitaonyeshwa kila siku kuanzia saa moja mpaka saa sita usiku, filamu zitakwenda sambamba na maonyesho ya muziki, upande wa pili wa ukumbi wa Ngome Kongwe.
Pati ya mwisho ya tamasha itafanyika siku ya wapendanao (Valentine Day) katika hotel ya Kendwa Rocks, kaskazini mwa zanzibar, kwa ajili ya wafanyakazi, waandishi wa habari na marafiki wa Busara.
Kuhusu Sauti za Busara Sauti za Busara inawapa fursa wanamuziki wa ndani kujifunza muziki kutoka sehemu mbalimbali za Afrika na wakati huo huo kuutambulisha muziki wa Afrika mashariki kwa wageni. Katika jamii yoyote fursa kama hii ni chache mno. Sauti za Busara inaandaa tamasha la mfano wa kuigwa kwa wenyeji na wageni, thamani ya kipekee na utajiri wa muziki kutoka Afrika. Inaonyesha uzuri wa utamaduni wetu katika ajira na kuongeza kipato.
Sanaa, warsha za ufundi na semina ni sehemu ya shughuli muhimu za Busara, lengo kuu ni kwa wanamuziki,wataalamu wa vyombo vya habari, mameneja wa sanaa na wafanyakazi wa sanaa. Warsha hizi zinasaidia kuongeza ujuzi na maarifa wa muda mrefu kwa watu wa Afrika mashariki.
Wadhamini wa Tamasha Sauti za busaraa 2012 linawezeshwa na: The Norwegian Embassy, HIVOS, Mimeta, Roskilde Festival Charity Society, Goethe Institut, The Embassy of France, Grand Malt, Toyota,Commercial Bank of Africa,African Leisure Centre, fly540, Memories, Zanzibar Grand Palace Hotel, Maru Maru Hotel, SMOLE II, Zanlink, Azam Marine, ZanAir, fRoots, Times FM,WOMEX, Multi-Color Printers, Ultimate Security, Southern Sun Dar es Salaam,Tabasam Tours, Emerson Spice, Monsoon Restaurant, Mercury's Restaurant,Archipelago Restaurant, Stone Town Café, http://www.zanzibar.net/.

No comments:

Post a Comment