KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, January 17, 2012

Primetime yaokoa jahazi Yanga


KAMPUNI Prime Time Promotion ya jijini Dar es Salaam imeingia mkataba na klabu ya Yanga ili
kuhamasisha mechi yake ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika dhidi ya Zamalek ya Misri, zinatarajiwa kukwaana nchini kati ya Februari 17 na 19 jijini Dar es Salam, kabla ya kurejeana kati ya Machi 2 na 4 huko Cairo, Misri.

Mwenyekiti wa Yanga Lloyd Nchunga amesema kuwa, kupitia mkataba huo, wataweza kutafutiwa wafadhili ambao wataiwezesha timu hiyo kufanya maandalizi yake kikamilifu, huku timu hiyo ikitarajiwa kuingia kambini jijini Mwanza wiki mbili kabla ya kuivaa Zamalek.

“Kama mnavyojua kwa sasa timu yetu ipo katika hali ambayo si nzuri ya kiuchumi hivyo kupitia
mkataba wetu huu wa ushirikiano na Primetime nadhani itasaidia kuokoa jahazi ili tuweze kujiandaa vizuri na hatimaye kushinda mechi zetu hizo.

“Napenda nichukue fursa hii kuwashukuru kampuni ya Primetime chini ya Mkurugenzi wake Mtendaji Joseph Kusaga ambaye kutokana na kuguswa na mkakati wa kusaka mafanikio ya soka kwa vilabu vya Tanzania wameona wajitokeze kutupa sapoti,”alisema.

No comments:

Post a Comment