KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, January 12, 2012

Kitwana Manara afiwa na mama yake

Marehemu Bi. Mishi Mikessy


Mwanasoka nyota wa zamani wa Tanzania, Kitwana Manara, amefiwa na mama yake mzazi, Bi. Mishi Mikessy.

Kitwana amisema mjini Dar es Salaam leo kuwa, mama yake huyo, anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 95, alifariki dunia jana usiku baada ya kuugua kwa wiki kadhaa.

Kwa mujibu wa Kitwana, mazishi ya Bi Mishi yanatarajiwa kufanyika kesho katika makaburi ya Waanglikana yaliyopo Buguruni-Malapa, Dar es Salaam.

Marehemu Bi. Mishi ameacha watoto watano na wajukuu kadhaa.

Kitwana ni kaka wa wanasoka wengine nyota wa zamani nchini, Sunday Manara na Kassim Manara.

Mkongwe huyo wa soka nchini, aliyezichezea klabu za Yanga, Pan African na Taifa Stars, anaomba taarifa hizi ziwafikie ndugu na jamaa popote walipo.

No comments:

Post a Comment