KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, January 12, 2012

Diamond awaomba msamaha Watanzania



Msanii wa Muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongo Fleva Diamond amewaomba msamaha Watanzania kwa kitendo ambacho kilitokea mjini Iringa na kusema kuwa hakitatokea tena.
Akizungumza na Kajunason Blog mara baara ya kutoka kufanya mahojino katika kipindi cha XXL cha redio Clouds jijini Dar es Salaam, Diamond alisema kuwa, "Nawaomba msamaha wapenzi wangu wa Muziki ikiwa ni pamoja na Watanzania wote kwa kitendo cha kumfanyia fujo mwandishi wa Iringa, Bw. Godwin Fransis.
"Unajua ni vyema kuwaomba msamahama watanzania kwa vile haikuwa dhamira yangu kumfanyia fujo mwandishi wa Iringa, Bw. Godwin Fransis bali ilitokana na hasira nilizokuwa nazo.
Mapema jana tarehe 4.1.2012 Diamond akiwa na wacheza show wake, walitolewa hukumu na hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Hakimu Masua alisema kulingana na watuhumiwa wote watatu kukiri kosa hilo anawahukumu kwenda jela miezi 6 au kulipa fidia ya shilingi elfu hamsini kila mmoja na huku wakilazimika kumlipa Godwin shilingi elfu 30 kila mmoja na kufanya kufikia kiasi cha shilingi 90,000 .

Wakitoa utetezi wao watuhumiwa hao walisema mahakama iwapunguzia adhabu kwa kuwa hawakukusudia kufanya kosa hilo, na wao walikuja mkoani hapa kwa ajili ya kutoa burudani, na kuwa tukio hilo wamelifanya kwa ghadhabu.

No comments:

Post a Comment