
NAHODHA wa timu ya soka ya taifa ya wanawake, Twiga Stars, Sophia Mwasikili akionyesha kitita cha sh. milioni saba, ambazo timu hiyo ilizawadiwa na wabunge kwa ajili ya malipo yao ya posho katika hafla iliyofanyika juzi kwenye uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja (kushoto) akiteta jambo la Mbunge wa Kawe (CHADEMA), Halima Mdee kabla ya kuanza kwa mechi ya kirafiki kati ya timu ya wabunge na timu ya taifa ya wanawake, Twiga Stars, iliyochezwa juzi kwenye uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam. Twiga Stars ilishinda mabao 2-1.
No comments:
Post a Comment