KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, February 6, 2012

VILLA SQUAD, SIMBA ZAINGIZA MIL 30/-



Mechi namba 107 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Villa Squad na Simba iliyochezwa Februari 4 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 30,017,000.

Watazamaji waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo ni 8,698 ambapo kiingilio kilikuwa sh. 3,000 kwa viti vya bluu na kijani, sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B na sh. 15,000 VIP A.

Baada ya kuondoa asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), ambayo ni sh. 4,578,864.41, fedha zilizobaki zilikuwa sh. 25,438,135.59.

Gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000. Posho ya kujikimu kwa mwamuzi wa akiba sh. 30,000, gharama za tiketi sh. 3,960,000, umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000.

Nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu ilipata sh. 608,860 wakati Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kilipata sh. 521,880.

Mgawo baada ya gharama za awali; uwanja na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kila moja ilipata sh. 1,503,853.56, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 751,926.78, gharama za mechi sh. 1,503,853.56, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 150,385.36, DRFA sh. 601,541.42 na kila klabu ilipata sh. 4,511,560.68.

No comments:

Post a Comment