KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, March 17, 2011

Banana azusha kasheshe na BASATA


KIONGOZI wa bendi ya muziki wa dansi ya B, Banana Zorro amezua mzozo kati yake na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), baada ya kudai kuwa, studio iliyofunguliwa na Rais Jakaya Kikwete itakuwa chini ya Chama cha Tanzania Fleva Unit (CTFU).
Akizungumza na waandishi wa habari wiki iliyopita, Banana alisema vyombo hivyo vya studio vipo chini yao na hakuna msanii yeyote atakayezuiwa kujiunga na chama hicho.
Banana, ambaye ni Makamu Mwenyekiti CTFU alisema, vifaa hivyo vipo chini yao pamoja na mtambo wa kufyatulia CD na kwamba vimehifadhiwa sehemu maalum.
"Tumeshampata prodyuza kutoka Uingereza, ambaye ni mtaalamu wa studio ya kisasa (master studio), baada ya wiki moja studio itafunguliwa," alisema Banana.
Hata hivyo, kauli hiyo ya Banana imepingwa vikali na Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego, aliyesema chama hicho hakisajiliwa na baraza hilo.
Materego alisema Chama cha Tanzania Urban Music (TUMA) ndicho pekee kinachotambuliwa na baraza hilo na ndicho chenye idhini ya kusimamia vyombo hivyo.
Alisema lengo la kuundwa kwa TUMA ni kukuza muziki wa kizazi kipya kwa lengo moja tu, hivyo hakuna sababu ya kuwa na vyama viwili.
“Huu ni muziki, sio siasa, vyama vingi havina manufaa kwa wasanii zaidi ya kuwatenga kwani kiliundwa chama kimoja kwa lengo la kushauri, kuhamasisha na kujenga umoja,”alisema.

No comments:

Post a Comment