KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, March 3, 2011

Mbaga kuzichezesha Simba na Yanga

Viingilio sh. 30,000 na sh. 3,000

MWAMUZI Oden Mbaga wa Dar es Salaam ndiye atakayepuliza kipenga katika mechi ya watani wa jadi wa soka nchini, Simba na Yanga.
Simba na Yanga zinatarajiwa kukutana keshokutwa katika mechi ya marudiano ya michuano ya ligi kuu ya Tanzania Bara, itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema mjini Dar es Salaam jana kuwa, Mbaga atasaidiwa na Mohamed Mkono wa Tanga na Maxmillian Nkongolo wa Rukwa.
Kwa mujibu wa Wambura, mwamuzi wa akiba katika pambano hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini atakuwa Mchungaji Army Sentimea wa Dar es Salaam.
Wambura alisema kiingilio cha chini katika mechi hiyo kitakuwa sh. 3,000 na cha juu kitakuwa sh. 30,000 kwa VIP A.
Alivitaja viingilio vingine kuwa ni sh. 20,000 kwa VIP B na sh. 10,000 kwa VIP B. Vingine ni sh. 7,000 kwa viti vya rangi ya machungwa n ash. 5,000 kwa viti vya bluu na mzunguko.
Ofisa huyo wa TFF alisema tiketi zitaanza kuuzwa kesho katika vituo vya Benjamini Mkapa, Big Bon Msimbazi, Steers Posta na Uwanja wa Uhuru.
Alisema maandalizi kwa ajili ya mchezo huo yapo katika hatua za mwisho na kuongeza kuwa, TFF inaamini mchezo huo utakuwa mzuri na wenye amani na utulivu.

No comments:

Post a Comment