KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, March 17, 2011

Marlaw, Besta sasa ni mume ne mke


HATIMAYE baada ya uchumba wa siri wa takribani miaka minne,mastaa wawili wa muziki wa kizazi kipya, Lawrence Marima ‘Marlaw’ na Besta Prosper Rugeiyamu wamefunga ndoa.
Marlaw na Besta walifunga ndoa mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye kanisa moja katoliki mjini Dar es Salaam na kufuatiwa na tafrija kabambe iliyofanyika kwa siri.
Habari kutoka kwa watu wa karibu na wanandoa hao zimeeleza kuwa, tafrija hiyo ilifanyika kwa siri kwa sababu hawakuwa wakitaka bughudha kutoka kwa watu.
Marlaw alikaririwa akiwaeleza baadhi ya rafiki zake kuwa, hakutaka harusi yao ipewe uzito kwenye vyombo vya habari kwa sababu ni suala la kifamilia zaidi.
Msanii huyo, anayetamba hivi sasa kwa kibao chake cha ‘Missing my baby’ alithibitisha kufanyika kwa harusi hiyo, lakini alikataa kuzungumza zaidi kwa kile alichodai ni mambo binafsi.
“Mahali tulipofungia ndoa ndipo hapo hapo tulipofanyia sherehe. Siwezi kuweka jambo hilo wazi kwenye vyombo vya habari kwa sababu ni suala la kifamilia zaidi,” alisema Marlaw.
Marlaw alisema ameamua kuachana na ‘ubachela’ na ameamua kumweka ndani Besta huku akimwomba Mungu awajalie maisha ya furaha.
Hata hivyo, Marlaw amewataka mashabiki wake wajiandae kusherehekea naye ndoa hiyo kwa utaratibu atakaowatangazia hapo baadaye.
Kabla ya kufunga pingu za maisha, familia ya Besta ilimwandalia tafrija kabambe ya kumuaga iliyofanyika wiki mbili zilizopita. Marlaw na Besta walikuwa wakificha uchumba wao kwa muda mrefu, lakini sasa wameamua kutimiza ndoto yao ya kuishi pamoja. Mungu awajalie maisha marefu.

No comments:

Post a Comment