KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Friday, March 25, 2011

WAREMBO WA UTALII WALIPOTINGA OFISI ZA UHURU

WAREMBO wa Miss Utalii wakiwa katika picha ya pamoja na Ofisa Utawala wa Kampuni ya Uhuru Publications Ltd, Rhoda Kangero walipotembelea ofisi za Uhuru mjini Dar es Salaam juzui

WAREMBO wa Miss Utalii wakisoma gazeti la Burudani walipotembelea katika ofisi za Uhuru juzi. Kushoto ni Mhariri wa Burudani, Rashid Zahor. Aliyeketi kulia ni mshindi wa taji la kipaji, Daisy Mushumbusi.



MWANDISHI wa habari wa gazeti la Burudani, Fred Majaliwa (kulia) akiwatambulisha warembo wa Miss Utalii kwa Mhariri wa Habari za Kimataifa wa gazeti la Uhuru, Noor Shija (aliyeketi).


MHARIRI wa Michezo wa gazeti la Uhuru, Mwadin Hassan (aliyeketi) akitoa maelekezo kwa warembo wa Miss Utalii.


MHARIRI Mtendaji wa Kampuni ya Uhuru Publications Ltd, Josiah Mufungo (kulia) akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na washindi watano wa kwanza wa shindano la kumsaka mrembo wa Utalii 2011 walipotembelea ofisi za Uhuru zilizopo barabara ya Lumumba mjini Dar es Salaam juzi
MHARIRI wa Habari wa gazeti la Uhuru, Ramadhani Mkoma (aliyeketi) akiwaonyesha warembo wa Miss Utalii jinsi habari zinavyopatikana kutoka mikoani kupitia mtandao wa kompyuta.

MENEJA Raslimali Watu wa Kampuni ya Uhuru Publications Ltd, Lucas Kisasa (kulia) akipeana mkono na mmoja wa washindi watano wa kwanza wa shindano la kumsaka mrembo wa Utalii walipotembelea ofisi za Uhuru mjini Dar es Salaam juzi.


WAREMBO wa Miss Utalii wakifuatilia kwa makini maelekezo waliyokuwa wakipewa na Msanifu Mkuu wa gazeti la Uhuru, Esta Mvungi (aliyeketi).

MHARIRI wa Makala wa gazeti la Uhuru, Epson Luhwago akitoa maelekezo kwa warembo wa Miss Utalii jinsi gazeti hilo linavyotengenezwa kwenye chumba cha kompyuta.

















No comments:

Post a Comment