KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, March 17, 2011

Keisha awa mama


MSANII nyota wa kike wa muziki wa kizazi kipya nchini, Khadija Shaban ‘Keisha’ amejifungua mtoto wa kiume hivi karibuni.
Akizungumza mjini Dar es Salaam wiki hii, Keisha alisema alijifungua mtoto huyo kwa njia ya upasuaji na ameamua kumpa jina la Jam Key.
Keisha alisema mtoto wake huyo ameshatimiza wiki tatu hapa duniani na anamshukuru Mungu kwa kujifungua salama.
“Kwanza namshukuru Mungu kwa kujifungua salama na kuweza kubeba dhamana ya kuitwa mama,”alisema msanii huyo huku uso wake ukiwa umepambwa kwa tabasamu mwanana.
“Hii itanifanya nizidi kujituma katika maisha yangu ili mwanangu aweze kuishi maisha mazuri hapo baadaye,” aliongeza.
Nyota huyo ambaye alifunika vilivyo kwenye wimbo wa ‘Bado tunapanda’ wa kundi la Tip Top Connection lenye maskani yake Manzese jijini Dar alisema alisema, pamoja na kupata kichanga hicho, bado ataendelea na kazi yake ya kukonga nyoyo za mashabiki.
Keisha alijiengua katika kundi hilo mwishoni mwa mwaka jana baada ya kutokea hali ya kutokuelewana kati yake na uongozi. Kwa sasa, Keisha anapiga muziki kwa kujitegemea.

No comments:

Post a Comment