KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, March 3, 2011

Mchunga: Mkutano Yanga ni baada ya ligi kuu

MWENYEKITI wa klabu ya Yanga, Llyod Nchunga amesema ataitisha mkutano mkuu wa wanachama baada ya kumalizika kwa michuano ya ligi kuu ya Tanzania Bara.
Akizungumza mjini Dar es Salaam jana, Nchunga alisema mkutano huo huenda ukafanyika Mei ama Juni mwaka huu na kuongeza kuwa, maandalizi yameshaanza.
Nchunga alisema kwa sasa hawawezi kuitisha mkutano huo kutokana na timu yake kukabiliwa na michuano ya ligi kuu, inayoelekea ukingoni.
Kwa mujibu wa Nchunga, mkutano mkuu wa Yanga unatakiwa kufanyika mara moja kwa mwaka, lakini wanaweza kuitisha iwapo kutatokea na dharula.
Alisema kwa sasa hakuna dharula yoyote inayoweza kusababisha waitishe mkutano huo, hivyo hawaoni sababu ya kufanya hivyo.
Uamuzi huo wa Nchunga umekuja baada ya baadhi ya wanachama kutaka uitishwe mkutano wa dharula kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayoihusu klabu hiyo.
Hatua hiyo ilikuja baada ya mfadhili mkuu wa klabu hiyo, Yusuf Manji kutangaza kujitoa kuifadhili timu hiyo kwa kile alichodai, kuandamwa na tuhuma mbalimbali.

No comments:

Post a Comment