KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, June 27, 2010

Ghana yaiua Marekani na kutinga robo fainali

ASAMOAH Gyan (kushoto) akishangilia na mchezaji mwenzake baada ya timu hiyo kuichapa Marekani mabao 2-1 jana katika mechi ya raundi ya pili ya michuano ya fainali za Kombe la Dunia.
MCHEZAJI Ayew wa Ghana (chini) akishangilia ushindi wa timu hiyo na mchezaji mwenzake baada ya timu hiyo kuishinda Marekani mabao 2-1.



MASHABIKI wa Ghana wakiserebuka katika mji wa Kumasi kushangilia ushindi wa timu hiyo jana dhidi ya Marekani.



BEKI John Mensah (kulia) wa Ghana akiwania mpira hewani na mshambuliaji wa Marekani, Deschamps timu hizo zilipomenyana jana katika mechi ya raundi ya pili ya michuano ya Kombe la Dunia. Ghana ilishinda mabao 2-1 na kufuzu kucheza robo fainali.

JOHANNESBURG, Afrika Kusini
GHANA juzi ilifuzu kucheza robo fainali ya michuano ya soka ya fainali za Kombe la Dunia baada ya kuichapa Marekani mabao 2-1 katika mechi ya raundi ya pili iliyochezwa mjini hapa.
Mshambuliaji Asamoah Gyan ndiye aliyeibuka shujaa wa Ghana baada ya kuifungia baoa la pili dakika ya tatu ya muda wa nyongeza wa dakika 30 baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 zikiwa sare ya bao 1-1.
Kipigo hicho kinamaanisha kwamba, safari ya Marekani katika fainali hizo imefikia ukingoni na itabidi isubiri hadi miaka minne iweze kujaribu tena bahati yake katika michuano hiyo mikubwa duniani.

Kevin-Prince Boateng aliifungia Ghana bao la kuongoza dakika ya 50 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Ricardo Clark na kufumua shuti lililompita kipa Tim Howard wa Marekani.
Landon Donovan aliisawazishia Marekani kwa mkwaju wa penalti dakika ya 62 baada ya beki Jonathan Mensah wa Ghana kumwangusha Clint Dempsey ndani ya eneo la hatari.
Katika mechi nyingine ya michuano hiyo iliyochezwa juzi, Uruguay nayo ilifuzu kucheza robo fainali baada ya kuichapa Korea Kusini mabao 2-1.

No comments:

Post a Comment