KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, June 15, 2011

Sina haraka ya kuolewa-Nwokoye



LAGOS, Nigeria
QUEEN Nwokoye, mcheza filamu wa Nollywood asiye na makuu amesema, hana papara ya kuolewa kwa sasa na kwamba atafunga ndoa pale atakapoona wakati wa kufanya hivyo umewadia.
Mcheza filamu huyo asiye na makeke alisema wiki hii kuwa, ndoa si kitu cha kuharakishwa kwa vile ni jambo linalopaswa kufanywa kwa umakini mkubwa.
“Sipendi kuolewa na baadae kuachika. Wazazi wangu wameoana miaka mingi na hadi sasa bado wanaishi pamoja na wanapendana,”alisema.
Hata hivyo, mwanadada huyo mwenye umbo la kuvutia hakuwa tayari kumtaja rafiki yake wa kiume kwa madai kuwa, hadi sasa anaishi peke yake.
“Kwa sasa, naishi peke yangu. Nipo makini, naishi peke yangu, lakini sitafuti mwanaume,”alisema.
Alipoulizwa iwapo amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji yeyote wa kiume wa Nollywood, Nwokoye alisema hajawahi kufanya hivyo.
Alisema wapo waigizaji wengi wa kiume wenye mvuto Nollywood, lakini si jambo zuri kuwa na uhusiano wa aina hiyo na mtu mnayefanyakazi pamoja.
Nwokoye alisema alianza kujitosa kwenye fani hiyo mwaka 2004 baada ya kumaliza shule. Alisema kamwe katika maisha yake hakuwahi kutarajia kuwa mwigizaji.
“Wakati wote nilipokuwa sule, kamwe sikufikiria kuwa mwigizaji. Lakini baada ya kumaliza shule na kukosa kazi, nilianza kufikiria mwelekeo huo,”alisema.
“Nilianza kutazama sinema. Hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kukaa chini na kutazama filamu ya Kinigeria. Nilianza kuvutiwa. Nilianza kwenda kufanya majaribio na hatimaye kupata nafasi,”aliongeza.
Nwokoye alisema anashukuru Mungu kwamba wazazi wake walimuunga mkono kuhusu uamuzi wake huo na mama yake alimweleza wazi kuwa, yeye ni mtu mzima anajua zuri na baya.

No comments:

Post a Comment