KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, June 9, 2011

Omotola adaiwa kuwa mpenzi wa bosi wa Sifax


NYOTA wa kike wa Nollywood, Omotola Jalade ameripotiwa kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Sifax Group, Taiwo Afolabi.
Omotola, ambaye ni mama wa watoto wanne, ameripotiwa kuwa na uhusiano na tajiri huyo kwa miaka minne na kwamba wamekuwa wakikutana kwa siri mno.
Gazeti moja la Nigeria liliripoti wiki iliyopita kuwa, Omotola amekuwa akimtembelea Afolabi ofisini kwake mara kwa mara kwa kisingizio cha kujadili masuala ya kibiashara.
Taarifa kuhusu uhusiano wa Omotola na tajiri huyo, zimevujishwa na rafiki mmoja wa karibu wa Afolabi na ambaye amekuwa akishuhudia mara kwa mara kukutana kwao.
Afolabi, ambaye miaka michache iliyopita alidaiwa kuwa na uhusiano na waigizaji wengine, Stella Damasus na Foluke Daramola, ameripotiwa kuwa hana mkono wa birika.
Mwishoni mwa mwaka jana, tajiri huyo wa jiji la Lagos aliliripotiwa kununua gani tano aina ya Jeep, ambazo alizitoa zawadi ya Krismasi kwa wake zake.
Juhudi za gazeti hilo kuwatafuta Omotola na Afolabi ili wathibitishe madai hayo, hazikuweza kupatikana.
Hata hivyo, hii si mara ya kwanza kwa Omotola kudaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume wa nje. Amekuwa akiripotiwa hivyo mara kadhaa, lakini mara zote amekuwa akikanusha.

No comments:

Post a Comment