KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, June 9, 2011

D'Banj: Mimi na Genevieve ni marafiki wa kawaida


LAGOS, Nigeria
MWANAMUZIKI nyota wa Nigeria, D’Banj amesema hana uhusiano wa kimapenzi na mcheza filamu, Genevieve Nnaji zaidi ya kuwa marafiki wa kawaida.
D’Banj alisema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akiwa ziarani nchini Malaysia, ambako alifanya maonyesho kadhaa ya muziki.
Kauli hiyo ya D’Banj ilikuja baada ya mmoja wa waandishi wa habari wa nchi hiyo kumtaka aeleze iwapo ni kweli ana uhusiani wa kimapenzi na mcheza filamu huyo nyota wa Nollywood.
Mwanamuziki huyo alisema taarifa zilizoripotiwa hivi karibuni na baadhi ya vyombo vya habari kwamba amemvisha pete ya uchumba Genevieve na kwamba wanatarajia kufunga ndoa Agosti mwaka huu si sahihi.
Alisema anatambua kuhusu kuwepo kwa uvumi huo, lakini alisisitiza kuwa yeye na mcheza filamu huo hawana uhusiano mwingine zaidi ya kuwa marafiki wa kawaida.
“Ni rafiki yangu mkubwa, sielewi uvumi huu unatoka wapi. Lakini siwezi kulalamika kwa sababu Genevieve ni mwanamke mrembo,”alisema.
Mwanamuziki huyo alikiri kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa ya Genevieve iliyofanyika hivi karibuni mjini London, Uingereza, lakini alisema alifanya hivyo akiwa mgeni mwalikwa na si mpenzi wake.
Hivi karibuni, wazazi wa D’Banj, prodyuza wake, Don Jazzy na Meneja wake, Sunday Are walisema hawana taarifa ya kuwepo kwa mipango ya harusi ya mwanamuziki huyo na Genevieve.
Wazazi wake hao walisema, kwa mujibu wa taratibu na utamaduni wa kabila lao la Yoruba, iwapo angekuwa na mipango ya kufunga ndoa na mwigizaji huyo, alipaswa kumtambulisha kwao kwanza.
Meneja wake, Are alisema D’Banj na Genevieve ni watu wazima na kwamba wanaweza kufunga ndoa iwapo watataka kufanya hivyo bila ya kuwepo kwa kikwazo chochote.

No comments:

Post a Comment