KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, June 9, 2011

Wazazi hawakupenda niwe mwigizaji-Monalisa


MSANII mahiri wa filamu wa Nigeria, Monalisa Chinda amesema wazazi wake kamwe hawakupenda ajihusishe na fani hiyo kwa kuiona haina mwelekeo mzuri kimaisha.
Akizungumza na mtandao mmoja wa nchi hiyo wiki hii, Monalisa alisema awali, wazazi wake hawakuifurahia kazi hiyo, lakini baadaye waliizoea na kuiona ya kawaida.
“Baba yangu hakuelewa kwa nini nilitaka niwe msanii kwa maisha yangu yote. Hakuiunga mkono kabisa fani hiyo wakati huo, lakini kwa sasa hana kinyongo, wameikubali na wanaona fahari juu yangu,”alisema.
Monalisa alisema licha ya kuwa na ngozi nyororo, hapendi kuacha wazi sehemu kubwa ya mwili wake wakati anapoigiza kwa sababu hiyo si desturi yake.
Alisema yeye ni mcheza filamu msomi na kwamba kazi yake haina uhusiano na mambo yake binafsi.
“Naweza kuigiza nafasi ya msichana mtukutu kwenye filamu, lakini siwezi kuonyesha sehemu kubwa ya mwili wangu,”alisema.
“Naweza kucheza filamu za mapenzi na kuonyesha vitendo vya kubusiana, lakini sifanyi hivyo kwa hisia. Najaribu kujenga mazingira ya mapenzi bila ya kuwa na hisia halisi kwa sababu hiyo ni kazi, tena ya kisomi,” alisema.
Monalisa alisema kamwe hawezi kuonyesha sehemu ya matiti yake katika filamu na kusisitiza kuwa, Wanigeria ni waafrika na kwamba kuna mambo yanayoweza kufanyika Ulaya, lakini hayapaswi kufanywa katika bara la Afrika.
“Mashabiki wameshaona sehemu ya kifua na mgongo wangu, wameshaona miguu yangu, wanataka nini kingine. Siwezi kuonyesha matiti yangu kwenye skrini kila mtu ayaone,”alisema.

No comments:

Post a Comment