KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, June 9, 2011

Sindodo yu buheri wa afya

MCHEZA filamu Tayo Odueke, maarufu kwa jina la Sikirat Sindodo,ambaye ilivumishwa kuwa yupo mahututi, ameibuka na hali yake imeelezwa kuwa ni nzuri.
Sindodo alionekana kwa mara ya kwanza Mei 22 mwaka huu katika sherehe ya siku ya kuzaliwa ya rafiki yake, Kemi Korede iliyofanyika katika kitongoji cha Egbeda mjini Lagos.
Kemi alithibitisha kuhusu kuwepo kwa Sindodo katika sherehe hiyo na kuongeza kuwa, mwanamama huyo amesharejea katika hali yake ya kawaida.
“Amerejea kwenye mwonekano wake ule ule mzuri na pengine amezidi kuwa mrembo,”alisema Kemi.
Mbali na kuripotiwa kuwa yupo mahututi, pia iliwahi kuvumishwa mara tatu kwamba Sindodo amefariki, lakini baadaye ikabainika kwamba, habari hizo hazikuwa za kweli.
Hivi karibuni, Sindodo aliripotiwa kuwa amelazwa katika hospitali ya Chuo cha Uuguzi cha Lagos kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa kansa.
Baadaye iliripotiwa kuwa, Sindodo alihamishiwa kwenye hospitali ya kanisa la T.B Joshua Synagogue kabla ya kuelezwa kuwa, alipelekwa nje ya nchi kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.
Kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa huo kwa muda mrefu, ilielezwa kuwa afya ya Sindodo ilikuwa mbaya na alipungua uzito kwa kiasi kikubwa.
Katika kipindi chote hicho, hakuna aliyeweza kukutana na mwigizaji huyo zaidi ya familia yake na rafiki zake wa karibu.

No comments:

Post a Comment