KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, June 9, 2011

RMD kumbe bado wamo


MCHEZA filamu mkongwe wa Nollywood, Richard Mofe Damijo kwa mara ya kwanza amepamba ukurasa wa mbele wa jarida jipya la Genevieve na kuzungumzia maisha yake ya kiusanii.
Richard, ambaye ni maarufu zaidi kwa jina la RDM, amepamba ukurasa wa mbele wa gazeti hilo katika toleo la mwezi huu, ambalo tayari lipo mitaani.
RMD alikuwa mmoja wa wacheza filamu maarufu wa Nigeria mwanzoni mwa miaka ya 1980. Ni mwigizaji wa kwanza wa nchi hiyo kulipwa naira milioni moja kwa kucheza nafasi ya mwigizaji mkuu.
Mchezaji filamu huyo, aliyeshinda tuzo nyingi, alianza kujipatia umaarufu mkubwa kupitia tamthilia ya Checkmate, ambayo aliicheza kwa kutumia jina la Segun Kadiri.
Hata hivyo, RMD hakudumu sana kwenye fani hiyo. Aliamua kuitosa na kwenda nje ya nchi kwa masomo zaidi ya chuo kikuu na baada ya kurejea Nigeria, aliteuliwa kuwa kamishna wa masuala ya utamaduni na utalii katika jimbo la Delta.
Alizaliwa Julai 6, 1961 katika kitongoji cha Warri kilichopo Jimbo la Delta. Mwaka 2005 alishinda tuzo ya mwigizaji bora ya Afrika. Alijitosa rasmi kwenye siasa mwaka 2009.
Mcheza filamu huyo pia aliwahi kufanyakazi ya uandishi wa habari katika magazeti ya Concord na Metro.
RDM alifunga ndoa na May Ellen Ezekiel, mwandishi wa habari maarufu wa zamani wa Nigeria, aliyekuwa akifahamika zaidi kwa jina la Mee. Mkewe huyo alifariki dunia mwaka 1996.
Kwa sasa, RMD ameoa tena na ana watoto wanne, wawili alizaa na mkewe wa kwanza na wengine wawili amezaa na mkewe wa sasa.

No comments:

Post a Comment