KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, June 9, 2011

Stephanie Okereke akana kuwa mja mzito


MWANADADA machachari katika fani ya uigizaji filamu Nigeria, Stephanie Okereke amekanusha madai kuwa ana uja uzito.
Stephanie alilieleza gazeti la Encomium wiki hii kuwa, anashangaa kusikia taarifa hizo zimeripotiwa tena kwenye vyombo vya habari kwa mara ya pili wakati si za kweli.
"Mimi nina uja uzito? Hii ni mara ya pili kusikia taarifa hizi. Nashukuru Mungu kwamba uvumi huu ni mzuri kwa sababu yeyote anayeusambaza, ananitakia mema,"alisema mcheza filamu huyo mwenye mvuto.
"Hizi ni taarifa nzuri na nawashukuru wale wote wanaonitakia heri. Lakini nasikitika kuwajulisha kwamba mimi sina uja uzito. Itatokea hivyo hivi karibuni, lakini kwa sasa, wote wanaonitakia mema, wanapaswa kusubiri itokee hivyo,"aliongeza.
Hivi karibuni, Stephanie alivishwa pete ya uchumba na mpenzi wake mpya, Linus Idahosa wa Kampuni ya Delyork.

No comments:

Post a Comment