KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, June 23, 2011

YAYA TOURE AONGOZA KWA UTAJIRI AFRIKA


LONDON, England
KIUNGO wa klabu ya Manchester City ya England, Yaya Toure anaongoza kundi la wachezaji wa Afrika wanaovuna fedha nyingi kutokana na kucheza soka.
Toure amechukua nafasi hiyo baada ya kuwapiku washambuliaji, Samuel Eto'o wa Cameroon, Didier Drogba wa Ivory Coast na Michael Essien wa Ghana.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Ivory Coast, pia anaongoza orodha ya wachezaji wanaolipwa fedha nyingi wanaocheza soka barani Ulaya.
Toure anakadiriwa kuwa na dola milioni 13.3 za Marekani (sh. bilioni 21.3). Katika orodha hiyo, kaka wa kiungo huyo, Kolo Toure, anayecheza pia Man City, anashika nafasi ya nne akiwa na dola milioni 10.3 (sh. bilioni 16.4).
Katika orodha ya majina manane ya wachezaji tajiri yaliyotangazwa jana, ni wachezaji wawili pekee wanaocheza soka nje ya England. Wachezaji hao ni Frederic Kanoute kutoka Mali, anayechezea klabu ya Sevilla ya Hispania na Mcameroon, Eto'o wa Inter Milan.
John Mikel Obi wa Chelsea, aliyewahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mwaka 2005, ametajwa kushika nafasi ya tano.
Jambo la kufurahisha zaidi ni kwamba klabu za Chelsea na Manchester City zimetoa wachezaji watatu kila moja kwenye orodha hiyo.
Orodha hiyo ni kama ifuatavyo:
1) Yaya Toure (Manchester City na Ivory Coast)

- dola milioni 13.3 (sh. bilioni 21.3)
2) Samuel Eto’o (Inter na Cameroon)

- dola milioni 12 (sh. bilioni 19.2)
3) Emmanuel Adebayor (Togo na Manchester City)

- dola milioni 12 (sh. bilioni 19.2)
4) Kolo Toure (Manchester City na Ivory Coast)

- dola milioni 10.3 (sh. bilioni 16.4)
5) Frederic Kanoute (Sevilla na Mali)

- dola milioni 8.6 (sh. bilioni 13.8)
6) Didier Drogba (Chelsea na Ivory Coast)

- dola milioni 8 (sh. bilioni 12.8)
7) John Mikel Obi (Chelsea na Nigeria)

- dola milioni 5.8 (sh. bilioni 9.3)
8) Michael Essien (Chelsea na Ghana)

- dola milioni 5.5 (sh. bilioni 8.8)

No comments:

Post a Comment