KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, June 15, 2011

Genevieve aibuka mwanamke mwenye mvuto

LAGOS, Nigeria
MWIGIZAJI nyota wa kike wa Nollywood, Genevieve Nnaji ameibuka mshindi katika kinyang’anyiro cha kuwania taji la mwanamke mwenye mvuto nchini Nigeria kwa mwezi Juni.
Genevieve alinyakua taji hilo kupitia mtandao wa NFC, ambao uliendesha upigaji kura kwa njia ya maoni kutoka kwa wasomaji mbalimbali.
Mwanadada huyo mwenye sura na umbo lenye mvuto, aliongoza baada ya kupata kura 225 na kumwaga mwigizaji mwingine nyota nchini humo, Omotola Jalade aliyepata kura 190.
Wanawake wengine waliofanya vizuri katika shindano hilo ni Mercy Johnson, aliyepata kura 175, Tonto Dikeh, aliyepata kura 100 na Omoni Oboli, aliyepata kura 70.
Genevieve ni mmoja wa waigizaji wanaolipwa fedha nyingi nchini Nigeria, akiwa anamiliki nyumba ya kifahari, magari ya starehe na jarida la mitindo na maisha.
Mwanadada huyo mantashau pia ni mwanamuziki na ameingia mikataba na kampuni mbalimbali za Nigeria kwa lengo la kutangaza bidhaa zao.
Alizaliwa Mei 3, 1979. Alianza kujihusisha na fani ya uigizaji mwaka 1998 kupitia filamu ya Most Wanted kabla ya kushinda tuzo ya mwigizaji bora wa Afrika mwaka 2005.
Mwanadada huyo, ambaye amebatizwa jina la Julia Roberts wa Afrika, alizaliwa Mbaise katika Jimbo la Imo na kukulia mjini Lagos. Ni mtoto wa nne kati ya watoto wanane wa familia yake.
Alianza uigizaji filamu akiwa mwigizaji mtoto katika tamthilia ya Ripples akiwa na umri wa miaka minane. Miongoni mwa filamu zilizompatia umaarufu ni pamoja na Last Party, Mark of the Beast na Ijele. Hadi sasa ameshacheza filamu zaidi ya 80.
Mwaka 2004 aliingia mkataba na Kampuni ya EKB Records ya Ghana kwa ajili ya kurekodi albamu yake ya muziki, inayojulikana kwa jina la One Logo logo line, ambayo imepigwa katika miondoko ya R&B na Hip hop.

No comments:

Post a Comment