KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, June 15, 2011

BHOKE: Hakuna ninachokijutia



MWAKILISHI wa Tanzania katika shindano la mwaka huu la Big Brother Amplified, Bhoke amesema hana anachokijutia kutokana na aliyoyafanya ndani ya jumba la Big Brother.
Bhoke alisema mjini Dar es Salaam wiki hii kuwa, alifurahia kuwa mmoja wa washiriki wa shindano hilo na pia kuwemo ndani ya jumba la Big Brother.
Mshiriki huyo wa Tanzania, alielezea msimamo wake huo, siku chache baada ya kutolewa katika shindano hilo.
Bhoke alitolewa sanjari na mshindi kutoka Uganda, Ernest. Inadaiwa kuwa, washiriki hao wawili walikuwa na uhusiano wa kimapenzi na walifanya ngono ndani ya jumba hilo.
Baadhi ya magazeti ya Tanzania na Uganda hivi karibuni yalichapisha picha zilizowaonyesha washiriki hao wawili wakifanya ngono huku wakiwa wamejifunika shuka.
“Sijutii chochote, kwa kweli nilifurahia kuwemo ndani ya nyumba na yote niliyoyafanya, niliyafanya kama mimi, hivyo hakuna chochote, ambacho naweza nikakijutia,”alisema.
Imedaiwa kuwa, Bhoke na Ernest walipigiwa kura nyingi za kutoka ndani ya jumbe hilo kutokana na kitendo chao hicho. Pia imedaiwa kuwa, washiriki wengi wa kike walikuwa wakimchukia Ernest.
Bhoke alikuwa miongoni mwa wawakilishi wawili wa Tanzania katika shindano hilo mwaka huu. Mwingine alikuwa Lotus, ambaye alikuwa wa tatu kutolewa baada ya kudaiwa alimpiga mshiriki kutoka Afrika Kusini, Luclay.
Washiriki wengine waliotolewa kwenye shindano hilo hadi sasa ni Michael (Msumbiji), Confidence (Ghana), Jossy (Namibia) na Nkuli (Afrika Kusini).
Waliopigiwa kura ya kutoka mwishoni mwa wiki hii ni Nic (Kenya), Luclay (Afrika Kusini), Kim (Zambia), Karen (Nigeria) na Danny (Ethiopia).

No comments:

Post a Comment